Hali ya usafiri kwenye Ziwa Kivu inaleta tatizo kubwa, ambalo lilisababisha ajali mbaya iliyotokea tarehe tatu Oktoba karibu na bandari ya Kituku huko Goma. Baada ya kuzungumza na walionusurika na familia za wahasiriwa, mwanabunge wa kitaifa mchaguliwa wa Masisi, Jules Mugiraneza anataja upakiaji wa kupitisha kiasi, hali mbaya ya boti lakini pia uzembe wa huduma za serikali. Tunampokea kama mwalikwa wetu wa siku hii. Anarejelea ushuhuda wa waathiriwa na dosari zinazoonekana katika sekta ya usafiri kwenye maji. Anazungumza na Sifa Maguru.

Source: Radio Okapi

By admin