Mgeni wetu ni Richard Kakule Kahwerikula, mkuu wa Kata Rwangoma ya manispa Beu katika mji wa Beni. Kiongozi huyo kimsingi anawasilisha kwetu hali ya sasa katika eneo lake, inayolengwa na mashambulizi ya waasi wa ADF kati ya elfu mbili kumi na sita na elfu mbili makumi mbili na moja, ambapo mamia ya raia walikuwa wameuawa. Pia anazungumzia athari za miradi ya maendeleo ambayo wakazi wa kitongoji chake walinufaika na MONUSCO. Richard Kakule akiongea na Grevisse Salumu.
Source: Radio Okapi